• Copy Image
    Enock Maregesi quote

    Musa alipokuwa mlimani kupokea Amri Kumi za Mungu kwa ajili ya Wana wa Israeli alikawia sana kurudi, kiasi cha watu kukata tamaa na kujiona wapweke wakiwa njiani kuelekea katika Nchi ya Ahadi. Kutokana na woga usio na kifani na kukata huko kwa tamaa waliamua kutosubiri tena kusikia neno kutoka kwa Mungu, au kuiona sura halisi ya Mungu kama Musa alivyokuwa amewaahidi, hivyo wakamlazimisha Haruni awatengenezee mungu kutokana na taswira ambayo tayari walishakuwa nayo vichwani mwao kuhusu mungu waliyemtaka; yaani ndama wa dhahabu, au mungu mpya ambaye angewapa chochote walichotaka muda wowote waliotaka

Moms Typewriter
A
A